Siasa

Uganda yaitaka YouTube kufungia vituo vilivyohusishwa na ghasi za Bobi Wine

Mamlaka ya mawasiliano nchini Uganda imeandikia Google, jukwaa la kushirikisha video, kuomba ifunge vituo 14 vinavyodaiwa kuhusishwa na ghasia za mwezi uliopita ambazo zilisababisha zaidi ya watu 50 kufa.

Ghasia zilizuka katika mji mkuu wa Kampala na miji mingine mikuu kufuatia kukamatwa kwa mgombea wa urais wa upinzani na mwanamuziki Robert Kyagulanyi, maarufu Bobi Wine, kwa kukiuka masharti ya kudhibiti ugonjwa corona.

Baadhi ya vituo vya YouTube vinavyohusishwa na Bobi Wine ndivyo vinalengwa, lakini mkuu wa masuala ya sheria wa Tume ya Mawasiliano ya Uganda ameambia kituo cha televisheni cha Bloomberg kwamba ni “bahati mbaya” tu.

Katika barua yake kwa Google,Tume hiyo ilisema vituo hivyo vilitumiwa kuchochea virugu na vinatangaza maudhui yanayokiuka sheria, Gazeti la Daily Monitor linaripoti.

Raia wa Uganda wanajianda kushiriki uchaguzi mkuu wa urais na ubunge Januari 14. Rais Yoweri Museveni, ambaye amekuwa madarakani kwa zaidi ya miongo mitatu, inataka kuchaguliwa tena.

Media hizo ni.

  1. Ghetto TV
  2. Map Mediya
  3. Busesa Media Updates
  4. Uganda Empya
  5. KK TV Uganda
  6. Ekyooto TV
  7. Bobi Wine 2021
  8. Namungo Media
  9. JB Muwonge
  10. TMO Online
  11. Lumbuye Fred
  12. Trending Channel Ug
  13. Uganda Yaffe
  14. Uganda News Update

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents