Habari

Uhalifu wapungua Dar kwa asilimia 2.6

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar ess Salaam imeeleza uhalaifu umepungua katika kanda hiyo kwa asilimia 2.6 ukilinganisha na mwaka jana.

Akizungumza leo Dar es Salaam Kamanda wa kanda hiyo, Lazaro Mambosasa Mambo amesema asilimia hiyo ni kutokana na kuwepo kwa upungufu wa makosa 3,405 kwa mwaka huu, 2017 ukilinganisha na mwaka uliyopita.

“Kuanzia January hadi November 2017 matukio ya uhalifu yaliyoripotiwa katika vituo vya polisi kanda maalum Dar es Salaam, jumla yake ni 126,200 ukilinganisha na kipindi kama hicho mwaka 2016 ambapo matukio yaliyoripotiwa yalikuwa 129, 602, hivyo kuna upungufu wa matukio 3, 405 sawa na asilimia 2.6,” amesema.

Pia ameongeza kuwa matukio makubwa ya kihalifu mwaka huu yalikuwa ni 9,736 wakati mwaka jana yalikuwa ni 12, 550 ambapo kuna upungufu wa makosa 2,815 sawa na asilimia 22. 4.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents