Bongo Movie

Ujanja wangu wote siwezi kuvaa kipini puani – Barnaba

Baada ya kuendelea kushamiri kwa mtindo wa wasanii kutoboa pua na kuvaa vipini, msanii na mtayarishaji wa muziki wa ‘High Table Sound’ Barnaba Classic amedai yeye hawezi kufanya kitu ka hicho katika maisha yake.
Barnaba

Akiongea na Bongo5 Jumamosi hii kuhusu kuboresha muonekano wake, Barnaba amesema atafanya kila kitu ili kuwa smart lakini siyo kutoboa pua.

“Muonekano kwa msanii ni kitu cha msingi sana, ndio maana kila siku Barnaba Classic nataka kuoneka classic na bado nitaendelea kuboresha muonekano wangu,” alisema Barnaba.

“Siwezi kutoboa pua au kuvaa kipini puani, ujanja wangu wote siwezi kufanya kitu kama hicho, kwa sababu siyo kitu ninachokipenda lakini nitafanya kila kitu kuhakikisha naoneka poa mbele ya watu,” aliongeza.

Diamond Platnumz ni miongoni kati ya wasanii ambae ametoboa pua hivi karibuni na kuvaa kipini.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents