Burudani

Ukubwa wa muziki haupimwi kwa namna unavyochezwa redioni tena – Godzilla

Rapper Godzilla amesema kuwa kuna ngoma nyingi ambazo hazifanyi vizuri redioni lakini mtaani zinapendwa na kusikilizwa na watu kwenye simu zao.

11357001_1840291556196675_1793457851_n

Rapper huyo amedai kuwa redio sio kipimo tena cha muziki kufanya vizuri kwa sasa. “Watu wanazo nyimbo kwenye simu zao, wanadownload na kusikiliza,” Godzilla ameiambia Bongo5.

“Ukiuweka kwenye internet watu wanadownload na kuwa nazo, ndio muziki ulivyokuwa siku hizi. Ukitaka kujua hilo ni ukienda kwenye show, watu wanaimba na wewe,” ameongeza.

“Kwahiyo sasa hivi ukubwa wa muziki haupimwi ni kwa jinsi gani umesikika kwenye redio au kiasi gani cha rotation unapata, watu wanazo nyimbo kwenye simu zao. Muziki umekuwa mpana kwamba watu wanaweza kupata muziki kwa njia nyingi, kwenye internet, kutumiana kwenye whatsapp group kwahiyo watu wanazo tu.”

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents