Burudani

Video ya Alikiba ‘Chekecha Cheketua’ yafikisha views zaidi ya laki 1 ndani ya saa 24

Video ya Alikiba ‘Chekecha Cheketua’ iliyokuwa ikisubiriwa kwa hamu na mashabiki wa muziki ndani na nje ya Tanzania imepata mapokezi mazuri toka ilipooneshwa kwa mara ya kwanza na Trace Urban.

Baada ya video hiyo iliyoongozwa na director Mnigeria, Meji Alabi na JM Films kuwekwa mtandao wa Youtube kwenye channel ya Alikiba, imepata views zaidi ya laki moja ndani ya saa 24.

Haya ni mafanikio kwa Alikiba ambaye kwa sasa yuko jijini Nairobi, Kenya akishiriki kwenye msimu mpya wa CokeStudio.

‘Chekecha Cheketua’ ni wimbo wa pili baada ya ‘Mwana’ kutoka kwa Alikiba akiwa chini ya ROCKSTAR4000.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents