HabariUncategorized

Waziri Ummy amuomba Mwanasheria Mkuu kubadili sheria watu waweze kujipima Ukimwi nyumbani

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe. Ummy Mwalimu amesema Wizara imemwandikia barua Mwanasheria Mkuu wa Serikali ili kubadili sheria na kila mtu aweze kujipima Ukimwi nyumbani.

Akizungumza Bungeni jijini Dodoma mapema leo wakati akijibu swali la nyongeza la Mbunge wa Mtambulie (CUF), Masoud Abdalla Salim ambaye alihoji kuhusu mikakati wa ziada wa Serikali kutambua wanaopata athari za Ukimwi.

Waziri Ummy amesema sheria imekuwa kikwazo kwa wananchi kujipima maambukizi ya Ukimwi hivyo sheria hiyo ilifanyiwa marekebisho kila Mtanzania ataweza kujipima Ukimwi mwenye nyumbani.

Waziri Mwalimu amesema, ni kweli maambukizi yameongezeka kwa mkoa wa Dodoma kutoka asilimia 2.4 hadi asilimia 5 sawa sawa na mkoa wa Tanga na Mwanza.

“Tunafanya utafiti maalumu kubaini kwa nini maambukizi yamepanda. Tumekuwa na changamoto ya kuwapata wanaume kupima na njia ya mtu kujipima mwenyewe,” amesema Waziri Mwalimu Kuhusu dawa za VVU, Waziri Mwalimu amesema, zipo kwa asilimia 100.

“Ukimwi si sentensi ya kifo, ukibainika tunakuingiza katika mpango wa kupata dawa.” amesema

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents