Bongo5 ExclusivesBurudaniDiamond PlatnumzHabari

Unahisi kwanini Diamond anashindanishwa na Chino kwenye muziki wa Amapiano??

Kupitia kipindi cha RECAP of & MANDO @el_mando_tz amezungumza kwa urefu kuhusu sakata la Chino Wana Man kutajwa sanna baada ya Diamond kuachia kionjo cha ngoma yake ya SHU ambayo hajaitoa bado.

@el_mando_tz ametujuza sababu za watu kumtaja sana Chino kwenye sakata hili la Diamond kusema ata-trend kutoka July mpaka January na baada ya hapo atamuachia msanii wake atrend.

Chino ndio msanii pekee aliyetrend baada ya kauli hiyo ya Diamond na mashabiki ndio wannaomtaja Chino wakidai kionjo cha SHU ya Diamond kuna namna kinaendana na AMAPIANO za Chino.

@el_mando_tz kwa upande wake ameeleza kuwa sio sahihi kabisa msanii chipukizi kama Chino kutajwa pale wimbo wa Diamond unaposikika kwa kuwa Diamond ni legend wa muziki wa Bongo Fleva.

Kwa upande mwingine amesema kuwa Diamond alikosea kuongea kauli kama ile kwani amewafanya wasanii wengi waanza kutoa kalu zisizo sawa mitandaoni wakidai wanaisubiria hiyo July.

Anasema ” Diamond kutoa kauli hiyo inaonyesha namna gani hajiamini kwa sasa kwenye upande wa muziki wake, kauli hiyo inaonyesha kuwa kuna wasanii ameingia wasiwasi kwao kutokana na wanavyofanya kazi zao.

Unahisi ilikuwa sahihi kwa msanii kama Diamond kuongea kauli ile??

 

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents