United, Liver katika vita kali ya nyota huyu wa RB Leipzig

Manchester United inaweza kujiunga na Liverpool katika mbio za kupata sahihi ya mlinzi wa kati wa RB Leipzig Ibrahima Konate. Mchezaji huyo,21 anatarajiwa kugharimu kiasi cha takribani pauni milioni 34. (Eurosport)

Ibrahima Konate

West Ham itajaribu kumsajili kiungo wa kati Jesse Lingard kwa mkataba wa kudumu msimu huu, lakini wanahofia Manchester United watataka dau la juu kumuachia mchezaji huyo mwenye miaka 28. (Mail)

Arsenal itafikiria kumuuza mshambuliaji wa Kifaransa Alexandre Lacazette katika dirisha la usajili katika majira ya joto. Inter Milan, Roma, Sevilla na Atletico Madrid zinataka kumnyakua mchezaji huyo mwenye miaka 29. (90min)

Alexandre Lacazette

Tottenham wanajiandaa na uhamisho wa kiungo wa kati wa RB Leipzig Marcel Sabitzer,27. (Football Insider)

Juventus, Arsenal na Chelsea wanamtolea macho kiungo wa kati wa AC Milan, Mturuki Hakan Calhanoglu, 27, ambaye anaweza kupatikana kwa uhamisho huru mwishoni mwa msimu. (Sky Sports-in Italian)

Mshambuliaji wa Villarreal Gerard Moreno, 28 ni miongoni mwa wachezaji muhimu msimu huu-hata hivyo gharama ya uhamisho ya Mhispania huyo ni pauni milioni 85.6 (Marca-in Spanish)

What a performance! Calhanoglu stars for Milan

Mshambuliaji Theo Walcott,32, atajiunga na Southmpton kwa mkataba wa kudumu , mara mkataba wake wa kucheza kwa mkopo Everton utakapokwisha (Talksport)

Everton itahitaji kiasi cha pauni milioni 21.4 ikiwa watamuuza mlinzi wa kati Yerry Mina (Team Talk)

Kocha wa Barcelona Ronald Koeman amemtaka mshambuliaji Ousmane Dembele,23, kusalia kwenye klabu hiyo, ingawa Manchester United imeonesha nia ya kumnyakua mchezaji huyo. (Metro)

Ousmane Dembele

Manchester City inamtolea macho kiungo wa kati wa Sheffield United Sander Berge,23,wakati wakitafuta mbadala wa kiungo wa Brazil Fernandinho,35, (Voelbal24-in Dutch)

Baba wa kiungo wa kati wa Uruguay Lucas Torreira ameitaka Arsenal kumruhusu mchezaji huyo, 25, anayecheza kwa mkopo Atletico Madrid, kuondoka kwenye klabu hiyo msimu huu.

Related Articles

Back to top button