HabariSiasa

Upinzani wasusia uchaguzi Tunisia

Watunisia leo Jumamosi wanapiga kura kuchagua bunge jipya.
Hata hivyo vyama vya upinzani vinasema uchaguzi huo unaofanyika chini ya mageuzi ya kujilimbikizia mamlaka mikononi mwa Rais Kais Saied ni kinyume cha sheria.
Vyama vya upinzani vimeamua kulisusia zoezi la kupiga kura.
Rais Kais Saied amebadilisha kwa kiasi kikubwa siasa za Tunisia kwa niaba yake tangu katikati ya mwaka 2021 ambapo amejipa karibu mamlaka yote.
Wakosoaji wanasema hilo ni sawa na utawala wa mtu mmoja na hivyo uchaguzi wa leo kwa kiasi kikubwa ni sawa na kulichagua bunge lisilo na meno.

Sheria hiyo mpya iliyopitishwa na rais Kais Saied  inahusu kupunguza idadi ya wabunge kutoka  217 hadi wabunge 161, ambao sasa watachaguliwa moja kwa moja badala ya orodha inayopendekezwa na vyama vya siasa.

Hivyo basi wabunge ambao hawatimizi wajibu wao wanaweza kuondolewa ikiwa asilimia 10 ya wapiga kura wao watawasilisha maombi rasmi ya kuondolewa kwa mbunge.

Related Articles

Back to top button