Habari

Urusi yavamia Ukraine ardhini, angani na majini, haijawahi tokea Ulaya tangu kumalizika kwa Vita Vikuu vya Pili  vya Dunia

Urusi imeanzisha leo uvamizi kamili nchini Ukraine kupitia ardhini, angani na majini. Hilo ni shambulizi kubwa kabisa kuwahi kufanywa na taifa moja dhidi ya jingine barani Ulaya tangu kumalizika kwa Vita Vikuu vya Pili vya Dunia.

Makombora ya Urusi yaliipiga miji mbalimbali ya Ukraine. Ukraine imeripoti msafara wa wanajeshi ikimiminika kwenye mipaka yake na kuingia katika maeneo ya mashariki ya Chernihiv, Kharkiv na Luhansk, na kutua baharini katika miji ya Odessa na Mariupol katika upande wa Kusini.

Hii ni baada ya Rais wa Urusi Vladmir Putin kukaidi shinikizo la kimataifa na vikwazo na kuzionya nchi nyingine kuwa jaribio lolote la kuingilia kati hali hiyo litasababisha madhara makubwa ambayo haziwajahi kuona.

Waukraine walianza kukimbia baadhi ya miji, na jeshi la Urusi limedai kuilenga na kuharibu miundo mbinu yote ya ulinzi wa angani wa Ukraine na vituo vya jeshi la angani. Rais Volodymyr Zelensky ametangaza sheria ya kijeshi kote nchini.

Source Deutsche Welle

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents