Habari

Utafunaji jojo kwa muda mrefu husababisha vidonda vya tumbo

Kuna athari kubwa sana zinazotokana na utafunaji wa bigijii (chewing gums) kwa muda mrefu.

Utafunaji huo husababisha tumbo kuzalisha acid ya kutosha likifikiri kuna chakula ambacho kinatafunwa tayari kumezwa. Kitendo cha kutafuna bigijii husisimua seli linazozunguka ukuta wa ndani wa tumbo kutengeneza juisi (digestive juice) ambayo husaidia kwenye mmeng’enyo wa chakula.

Hii ni njia asilia ambayo husababisha chakula ambacho kimetafunwa kuanza kumeng’enywa punde tu kinapofika tumboni. Kwahiyo utafunaji wa bigijii (chewing gums) husababisha uzalishaji wa aside isiyo na ulazima. Hii ni habari nmbaya kwa walaji wa bigijii kwani aside hii huongeza athari za kupata vidonda vya tumbo.

Lakini risk ni ndogo sana labda uwe unatafuna bigijii (chewing gums) nyingi sana kwa siku, kwahiyo ondoa hofu labda uwe kocha wa mpira wa miguu (football coach).

Your Health, Our Concern

FORD A. CHISANZA
Scientist/Researcher/pharmacist
Location: Off Mandela Road, Mabibo – External,
P.o.Box: 77150, Dar Es Salaam, Tanzania.
Mobile:+255 652466430/+255 684363584
Email: [email protected]

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents