HabariMichezo

Uwanja wa Benjamin Mkapa kufungwa

Shirikisho la soka Afrika (CAF) limeshauri kutotumika Dimba la Benjamin Mkapa ili kufanyiwa marekebisho kwa kile wanachodai kuwa eneo la kuchezea (pitch) limeharibika.

Baada ya mchezo wa Ligi Kuu ya NBC utakochezwa leo kati ya Yanga SC na KMC FC, Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam utafungwa kwa mwezi mmoja kupisha marekebisho hasa kwenye eneo la kuchezea.

Meneja wa uwanja huo Salum Mtumbuka amesema kuwa baada ya michezo miwili ya mashindano ya Afrika mwishoni mwa wiki walikutana na maafisa wa Shirikisho la Soka Afrika ambao waliwapa maelekezo ya kufanya marekebisho hayo.

“Tulikubaliana na CAF wakati marekebisho yanaendelea, mechi zitakazochezwa hapo labda zile za kimataifa za CAF na timu ya Taifa. Mechi nyingine za ligi kuu watatumia Uwanja wa Uhuru au viwanja vingine,” amesema Mtumbuka

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents