Habari

Uwanja wa KIA kupokea ndege 11 kwa mara moja

Mamlaka ya Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA) imesema kuwa wanatarajia uwanja huo kupokea ndege kubwa zaidi ya 11 kwa mara moja pindi ukarabati utakapo kamilika.

img_2170-1024x683

Meneja wa upanuzi wa uwanja huo, Mhandisi Mathew Ndossi amekiambia kituo cha runinga cha ITV kuwa siku chache zijazo uwanja wa KIA utakuwa ni miongoni mwa viwanja vikubwa vyenye uwezo wa kupokea abiria wengi na ndege nyingi kubwa hali itakayofanikisha uwanja huo kuingiza fedha za kigeni

Aidha meneja huyo ameongeza kuwa uwanja wa KIA utaweza kupokea zaidi ya abilia milioni 1 kwa mwaka na kutua ndege kubwa kumi na moja kwa wakati mmoja.

Kwa sasa mradi huo unaenda pamoja na ufungaji wa vifaa vya kisasa ili kudhibiti uhalifu uwanjani hapo.

BY: EMMY MWAIPOPO

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents