Uwizi katika Ubalozi wa China

parking

Baadhi ya wafanyakazi wa ubalozi wa China, jijini Dar es Salaam, wanadaiwa kushirikiana na wezi wa kuvunja magari ya watu wanaofika ubalozini hapo.

Kumekuwa na matukio ya uhalifu katika ubalozi huo na bongo5 ilitembelea eneo hilo na kukuta vijana wakizagaa hovyo nje ya jengo la ubalozi hasa katika eneo la maegesho ya magari ambako uhalifu huo unafanyika.

Baadhi ya watu ambao wamekumbwa na mkasa wa kuibiwa katika eneo hilo la maegesho ya magari ubalozini hapo walisema watu wanaofanya uhalifu huo ni wa rika tofauti tofauti na wamekuwa  wakivinjari katika ubalozi huo bila shughuli yoyote muhimu.

Katika tukio la hivi karibuni, gari la Mkurugenzi Mtendaji na mmiliki wa maduka ya vipodozi ya Shear Illusions Shekha Nasser, lilivunjwa na kuibiwa Laptop moja, fedha taslimu kiasi cha sh 250,000, tiketi ya ndege moja  na vitabu vya hundi viwili vya benki ya CRDB na NMB, funguo za maduka na vitu vingine mbalimbali.

Shekha alisema tayari amefungua jalada lenye RB OB/RB/21477/2010 katika kituo cha Polisi Oysterbay, Dar es Salaam.

Kwa mujibu wa Shekha, mara baada ya kuibiwa alimueleza mlinzi aliyekuwepo katika ubalozi huo, lakini jambo la kushangaza alimjibu kuwa hashangazwi na tukio hilo kwani vitendo hivyo vimeota mizizi na kukiri kwamba kwa siku huwa watu watano hadi sita huibiwa na kazi ya kulinda magari siyo ya kwao bali ni ya Jeshi la Polisi.

Kadhalika watu wanaoranda randa katika ubalozi huo wanadai kuwa wao ni mawakala wa kusaidia watu kupata pasi za kusafiria.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents