Burudani

Video: Beka (Natumaini) kuja na album aliyoimba kwa makabila zaidi ya matano

Muimbaji mahiri wa muziki aliyewahi kutamba na wimbo ‘Natumaini’, Beka Ibrozama, anatarajia kuja na album mpya iitwayo Kwetu aliyoimba kwa zaidi ya makabila matano.

Katika makabila hayo hakuna hata moja la kwake.

Ameiambia Bongo5 kuwa ukimya wake ulisababishwa na kuwa busy kuiandaa album hiyo na pia kutengeneza bendi yake itakayoanza hivi karibuni.

“Nimechukua muda mwingi kuitengeneza kwasababu nimeenda lugha kama tano tofauti,” amesema.

“Nimeimba Kinyakyusa, nimeimba Kichaga, nimeimba Kiha, nimeimba Kimanyema, nimeimba Kisukuma,” ameongeza.

Amesema kuwa ilimchukua zaidi ya miezi mitatu kuweza kuimudu kabila moja na kuyatamka matamshi kwa ufasaha. Katika kuandika nyimbo hizo Beka aliziandika kwa Kiswahili na aliwatafuta watu wa makabila hayo wakamtafsiria na yeye kutafuta sauti mwenyewe.

Amesema album hiyo imekamilika na inahadhitia mambo mbalimbali ya Tanzania.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents