Burudani

Video: Beyonce hakuimba live wimbo wa taifa wakati wa kuapishwa kwa Obama (alilip-synch)

Pamoja na kuonekana kuimba wimbo wa taifa wa Marekani kwa ustadi mkubwa juzi wakati wa kuapishwa kwa Rais Barack Obama, imebainika kuwa Beyonce aliamua katika dakika za mwisho kutoimba live na badala yake kukandamizia kwenye wimbo aliourekodi awali (lip-synch).

Kwa mujibu wa msemaji wa bendi ya jeshi la maji la Marekani iliyokuwa ikipiga vyombo vya muziki wakati Beyonce akiimba, mshindi huyo wa Grammy aliamua kutumia wimbo uliorekodiwa akimaanisha kuwa hakuwa akiimba live.

Maelezo hayo yanasema kuwa bendi hiyo na Beyoncé, hawakuwa na nafasi ya kufanya mazoezi kabla ya sherehe hizo za juzi Jumatatu na hivyo kuimba live ulikuwa ni uamuzi wa hatari kwenye tukio kubwa kama lile.

Hata hivyo kwa mujibu wa mwanamuziki Aretha Franklin, hali ya hewa ya siku hiyo haikuwa nzuri kwa kuimba live na ameunga mkono uamuzi huo.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents