Habari

Video: Dereva wa Lissu akirudi Tanzania anaweza akauwawa – Mhe. Mbowe

Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Freeman Mbowe ambaye ndiye mwenye mamlaka ya kuizungumzia afya ya Mbunge, Tundu Lissu aliyeshambuliwa kwa risasi na watu wasiojulikana, amesema hali ya mwanasiasa huyo inaendelea vizuri huko nchini Kenya anapopatiwa matibabu.

Akizungumza na kitengo cha habari cha chama hicho, Mbowe amelikataka jeshi la polisi nchini kuongeza kasi ya upelelezi huku akidai dereva ambaye alikuwa anamuendesha Mbunge huyo wa Singida anaendelea na matibabu ya kisaikolojia ambapo pia amedai wanaogopa kumrudisha nchini Tanzania kutokana na hali ya usalama.

“Kwa sababu leo ni siku 32 zimepita jeshi la polisi linasema linamsubiri dereva wa Lissu lifanye uchunguzi, dereva wa Lissu tupo naye Nairobi anaendelea kupatiwa matibabu ya kisaikolojia kwa sababu aliona tukio lakutisha na vile vile kumrejesha Tanzania katika hali ambayo hatujapewa uhakika wa usalama wake, wanaweza bado wakamuua, wakamtoa roho yake, ndio maana tukasema lazima tumlinde kama tunavyomlinda Mhe Lissu kule hospitali analindwa na maaskari wenye bunduki,” alisema Mbowe.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents