Michezo

Misri ya tinga fainali ya michuano ya kombe la dunia Urusi 2018

Timu ya taifa ya Misri imetinga fainali ya michuano ya kombe la dunia inayotarajiwa kufanyika nchini Urusi hapo mwakani baada ya kuchomoza na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Congo.

 

Mapharao hao wameibuka na ushindi kunako dakika ya 95 baada ya kupata goli la pili kupitia kwa mchezaji wao anaekipiga katika klabu ya Liverpool ya nchini Uingereza, Mohamed Salah mchezo uliyochezwa hapo jana usiku katika dimba la Borg El Arab huko Alexandria.

Kwa ushindi huo sasa unaiweka Misri katika uongozi wa msimamo wa kundi E ikiwa na jumla ya pointi 12.

Timu ya taifa ya Uganda ambayo imetoa sare ya bila kufungana dhidi ya Ghana siku ya Jumamosi inashika nafasi ya pili kwa kuwa na jumla ya point nane wakati Ghana yenyewe ikishika nafasi ya tatu na Congo ikiburuza mkia kwa alama moja katika kundi hilo la E.

Mabao ya Misri yamefungwa na Mohamed Salah dakika ya 63’ na lapili likifungwa kwanjia ya mkwaju wa penati dakika za nyongeza ya 95.

Bao pekee la Congo limefungwa na  Moutou dakika ya  88

Nigeria yaungana na timu 11 kuelekea Kombe la Dunia 2018

 Kikosi cha timu ya Misri ni  El Hadary, Hegazy, Fathi, Abdelshafi, Rabia, Elneny, Hamed, Sobhi (Elmohamady 88’), Salah, Hassan (Gamal 78’), Gomaa (Mahmoud 56’).

Kikosi cha timu ya Congo Mouko, Itoua, Mayembo, Etou, Badila, N’dinga, Saint-Louis (Gandze 93’), Delarge (Bouka Moutou 71’), Oniangue, Bahamboula (Ndockyt 84’), Bifouma.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents