Burudani

Video: ‘Hawajui’ ya Vanessa Mdee kuongezwa kwenye soundtrack ya filamu ya Going Bongo, video itatumia scenes za filamu hiyo

Wimbo mpya wa Vanessa Mdee, Hawajui utajumuishwa kwenye soundtrack ya filamu ya Going Bongo, imefahamika.

https://www.youtube.com/watch?v=LR50Tby8fYQ

Vanessa ambaye anadaiwa kuanza kushoot video ya wimbo huo ulioandikwa na Barnaba na kutayarishwa na Nahreel, anaweza pia kuchanganya na baadhi ya scenes kutoka kwenye filamu hiyo iliyochezwa na Mtanzania, Ernest Napoleon na wasanii wengi wa Marekani, Kenya na Tanzania.

Akiongea na Bongo5, Napoleon amesema kuna uwezekano wa wimbo wa Vanessa Mdee kujumuishwa kwenye album ya soundtrack itakayouzwa kupitia iTunes. Wimbo wa marehemu Ngwair, ‘Nipeni Deal’ upo pia kwenye soundtrack ya filamu hiyo.

Going Bongo ndio filamu ya kwanza Afrika Mashariki kuuzwa kupitia mtandao wa iTunes.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents