Burudani

Video: Jaguar amponda Iyanya, ‘I don’t pick his phone’

Pamoja na kumshirikisha kwenye remix yake ya One Centimeter, Jaguar haziivi tena na Iyanya.

Akiongea kwenye tuzo za Bingwa zilizotolewa jana jijini Nairobi ambapo alishinda tuzo ya video bora ya mwaka, Jaguar alisema Iyanya alimpa masharti kuwa kama anataka washoot video hiyo ni lazima waende Nigeria ama Uingereza na wawatumie waongozaji wa Nigeria, Clarence Peter au Moe Musa. Jaguar anadai kuwa aliamua kwenda Nigeria akiwa na muongozaji wake na kufika huko Iyanya alitaka kugoma kama Clarence.

“Nikamwambia hata mimi si lazima tufanye hii video,” alisema Jaguar na kuongeza kuwa Iyanya alikuja kubadili mawazo baada ya muda.

Baada ya video kutoka alimtumia video hiyo Iyanya ili avipe vituo vya TV vya Nigeria lakini aliona kimya na ndipo alipoamua kumuuliza mtu mwingine wa Nigeria aliyesema TV za huko haziwezi kucheza video zaidi ya zile za wasanii wao.

“I don’t pick Iyanya’s phone,” alisema msanii huyo. “Even if Iyanya akinipigia simu leo sipokei simu yake.”

Jaguar pia aliwaasa Wakenya kuunga mkono muziki wa Kenya.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents