Burudani

VIDEO: Kwa uwezo huu wa mtoto wa P. Diddy ‘King Combs’ hakuna ubishi kuwa ndiye atakayerithi mikoba ya Bad Boy Records

Wahenga wanasema mtoto wa nyoka ni nyoka hawezi kuwa chura kamwe na msemo huu unakuja kudhihirika kwa mtoto wa rapper P. Diddy, Christian Casey Combs maarufu kwa jina la King Combs.

Combs ambaye mara kwa mara anaonekana mara kwa mara kwenye mitandao ya kijamii akiposti vipande vya video akirap kwa sasa tayari ameshaingia rasmi kwenye tasnia hiyo kwa kuachia ngoma yake ya kwanza na kuwashirikisha mastaa wakubwa nchini Marekani DJ Khaled na Chris Brown.

Wimbo huo unaoitwa ‘Love You Better’ ambao umeachiwa wiki iliyopita mpaka sasa video yake imetazamwa mara milioni 1.

Kati ya watoto watano wa P. Diddy, Combs ndiye mtoto pekee wa rapa huyo ambaye anaonekana kufuata nyayo za Baba yake kwenye muziki.

Hata hivyo, baba yake aligundua kipaji cha King Combs mapema kabisa kwani mwaka 2016 alipofikisha miaka 18 alitangaza kumsaini kwenye lebo yake ya Bad Boy Records ingawaje hakutoa wimbo wowote mkubwa kwa miaka yote miwili tangu asainiwe.

P. Diddy na King Combs

Tayari majarida makubwa duniani kama jarida la Complex limeshamtabiria mafanikio makubwa zaidi huku likimtaja King Combs kama mtoto pekee mwenye uwezo wa kuiendesha Bad Boy Records hata kama baba yake akiamua kuachana na masuala ya muziki.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents