Bongo Movie

Video: Mayunga azungumzia ukimya wake pamoja na label zinazomnyatia kumsaini

Mshindi wa shindano na Airtel Trace Music Star 2015, Mayunga amesema ukimya wake kwenye muziki unatokana na maandalizi ya kazi zake mpya ambazo zitatoka siku za usoni.

Muimbaji huyo ambaye pia anawania tuzo ya mwanamuziki bora chipukizi wa EATV Award 2016, ameiambia Bongo5 kuwa yeye pamoja na uongozi wake wapo katika maandalizi ya ujio mpya.

“Harakati zinaendelea kwenye muziki sema nilikuwa kimya kutokana na maandalizi ya kazi mpya ili kujiweka vizuri zaidi katika tasnia ya muziki,” alisema Mayunga. “Kwasasa hivi kuna kazi ambazo zipo tayari zitatoka pale management yangu itapoamua kuziachia kwa sababu wao ndio wanasimamia kila kitu kwenye muziki,”

Kwa upande wa management zinazomnyatia, Mayunga alisema “Hakuna label ambayo inataka kunisaini lakini wapo ambao wanataka kufanya kazi na mimi kama partner kwa sababu mimi nipo chini ya Trace ambao wanajukumu la kusimamia kazi zangu,”

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents