BurudaniVideos

Video: Navy Kenzo watangazwa mabalozi wa app ya Klobaa, wazungumzia tamasha la Mwendo Kasi

Kundi la muziki la Navy Kenzo linaloundwa na Nahreel na Aika limechaguliwa kuwa mabalozi wa app ya Klobaa, kampuni iliyoanzishwa Marekani mwaka 2015 na sasa ikiwa imesajiliwa kufanya biashara nchini.

Noma

Klobaa ni app inayowaunganisha watumiaji na matukio mbalimbali ya burudani na matukio ya usiku katika majiji mbalimbali na itazinduliwa rasmi Jumamosi kwenye tamasha la Mwendo Kasi. Akiongea na waandishi wa habari Ijumaa hii, Perrycurtis Elechi wa Klobaa amedai kuwa waliamua kuwachukua Navy Kenzo kama mabalozi wao kutokana na hatua kubwa kimuziki waliyofikia.

“Tuliwasikia wawili hawa mara ya kwanza mwaka 2015 na tumekuwa tukiwafuatilia tangu muda huo kwa mtazamo wa kuja kufanya kazi kwa ukaribu,” alisema Elechi.

“Hadi sasa tumependezwa na hatua waliyoipiga kama brand na ukuaji ukuaji kama watu mashuhuri kila mmoja,” aliongeza.

Aliongeza kuwa wanapendezwa na jinsi wasanii hao wanavyojituma na wanavyoendelea kulikuza kundi lao barani Afrika. Huo unakuwa ubalozi wa pili kundi hilo unapata mwaka huu baada ya ule wa kampuni ya simu ya Airtel kupitia kampeni yake ya Yatosha.

Akiongea kwenye mkutano huo, member wa kundi hilo Aika, amedai kuwa kuchaguliwa kama mabalozi wa Klobaa ni ishara ya jinsi muziki wa Tanzania ulivyokuwa mkubwa.

“Kampuni kama hizi zinapokuja kwenye nchi yetu kuangalia ile quality ya vitu ambavyo wanataka. Wana mipango mingi sana ya kwenda na sisi mpaka duniani kwasababu wameona kipaji chetu kinapoelekea ni kitu ambacho kinaweza kika take over the world na sisi tunafurahi kupata hiyo chance,” alisema Aika.

“Tutazunguka nao, tumeanza hapa Tanzania, tumepewa hii privilege kubwa na sisi tunashukuru Tanzania tumekuwa wa kwanza kuilaunch hii app, then tukitoka hapa tutaenda Uganda, Kenya, Kigali, Dubai, Marekani, Uingereza na tutakuwa nao. Hiyo pia itatusaidia kuonesha talent yetu kutumia hii endorsement ambayo tumepata,” alisema Nahreel.

Pia wamezungumzia tamasha la Mwendokasi litakalofanyika kwenye viwanja vya Posta Kijitonyama litakalohusisha orodha ndefu ya wasanii. “Tunataka tuvunje rekodi, tumepanga show kubwa sana, tunataka watu wanaokuja hapa wasema ‘yes’ Navy Kenzo wanastahili hiyo chance,” alisisitiza Aika.

Wasanii wengine watakaotumbuiza kwenye show hiyo ni pamoja na kundi la Sauti Sol la Kenya, Alikiba, G-Nako, Juma Nature, Joh Makini, Roma, Snura, Isha Mashauzi, Barnaba na wengine.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents