BurudaniVideos

Video: Producer wa Aiyola ya Harmonize aeleza alivyotafutwa na msanii wa Nigeria, Olamide

Maximizer ni producer aliyetayarisha hits kibao ambazo huenda ulikuwa hujui.

Hits hizo ni pamoja na Siri ya Vanessa Mdee na Barnaba, Pacha Wangu ya Rich Mavoko, Aiyola na Kidonda Changu za Harmonize, For You ya Q-Chief, Sielewi ya Chemical na zingine kibao. Hata hivyo Aiyola ya Harmonize ndiyo iliyompa channel zingine kubwa.

Miongoni mwao ni kutafuta na staa wa Nigeria, Olamide.

“Olamide alisikia kazi yangu Aiyola, nafikiri alipoisikia akawa anamtafuta producer aliyeiproduce. Baada ya kunitafuta katika mitandao akanisearch pale,” amesema Maximizer.

“Nikakuta tu direct message kwenye Instagram. Kwanza sikuamini, nikaifungua ile profile yake nikaona ndio mwenyewe. Akajaribu kunitumia email yake na mimi nikamtumia sababu tunatumia email ya ofisi pale anaendesha Lawize ambaye ni meneja wa studio pale. Akanitumia email akawa anachat na uongozi wa Kazi Kwanza ‘ebana nyimbo Aiyola imetengenezwa wapi’ akaulizia mastering na mixing, nikamuambia kila kitu nimemaliza.”

Anasema Olamide alimuomba amtumie nyimbo zingine alizotayarisha na hapo ndipo alipoamini kuwa producer huyo anaweza. “Nikamtumia akasema yes kuna kitu nimekiona.”

Olamide alimuambia kuwa anaweza kufanya naye kazi kwakuwa anatarajia kuja Afrika Mashariki hivi karibuni na kama ikishindikana atamtumia beat afanye huko huko.

Maximizer amesema akifanya kazi na Olamide ana uhakika wa jina lake kufahamika zaidi barani Afrika.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents