Bongo Movie

Video: Richie azieleza sababu mbili za kushuka hadhi kwa tamthilia za TV nchini

Unakumbuka enzi za Mambo Hayo, Kaole, Kidedea na Jumba la Dhahabu jinsi tamthilia za TV zilivyokuwa zikipendwa nchini? Tamthilia hizo ndio zilizalisha asilimia kubwa ya mastaa wa filamu leo hii. Kanumba, Ray, JB, Richie, Tino, Monalisa, Natasha na wengine wengi wote walianzia huko.

Lakini hali imebadilika sasa, hakuna tena vikundi vyenye tamthilia za maana kwenye TV za Tanzania, kwanini iko hivyo? Richie anayo majibu.

“Wakati ule sisi tulionekana tofauti sababu tulikuja na something new,” anasema Richie ambaye umaarufu wake ulitokana kuigiza kwenye tamthilia ya Mambo Hayo akiwa na waigizaji wengine kama Bishanga Bashaiga, JB, Waridi na Aisha.

“Kwahiyo wanachokifanya sasa hivi ni kile ambacho tulishakifanya zamani, kwahiyo kunakuwa hakuna mpya watu wanachoka kuangalia, that’s number one. Number 2 hawapewi nafasi, nafasi ya kufanya kwa muda kiasi. Kikundi kinapoanza vizuri, wanapoanza wanakuwa kama malearner, wanapoanza kukaa vizuri basi ile airtime wananyimwa wanaletwa tena wengine wanakuwa tena amateur tena, wanapotaka kuanza kutake vizuri nao tena wanakosa ile airtime.”

Richie amesema kuigiza kwenye tamthilia za TV hakuna kipato kabisa lakini kunasaiadia wasanii wachanga kupata jina na hivyo kuwa rahisi kufanikiwa kwenye filamu.

“Kila siku sisi tunawaambia hata watu wanaokuja kwenye film wanataka kulipwa sawa na watu wengine lakini hawajui sisi tulisota muda gani, sisi tulisota kama wao. Tunawafundisha kila siku kwamba unatakiwa utafute nafasi, baada ya kutafuta nafasi utafute jina baada ya kutafuta jina utafute pesa. Kwahiyo sasa wao wanataka kuanza na pesa ndio inapokuwa ngumu sana hapo.”

Katika hatua nyingine, Richie amesema kwa sasa yupo kwenye matayarisho ya mwisho (post production) ya filamu yake ijayo, Kitendawili.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents