Videos

Video: Serikali yasita kumbeba Dangote kuepuka kuviathiri viwanda vingine vya saruji

Waziri wa viwanda, biashara na uwekezaji, Charles Mwijage amesema serikali haina mvutano na kiwanda cha kuzalisha saruji cha Dangote kutokana na mawasiliano waliyoyafanya kabla ya kufungwa kwa kiwanda hicho na kuwa wanakabiliwa na matatizo ya kiufundi.

pix-1

Akizungumza na waandishi wa habari Waziri Mwijage ametoa ufafanuzi wa mvutano huo kati ya serikali na kiwanda cha Dangote na kudai kuwa kukipendelea kutasababisha kuanguka kwa viwanda vingine.

“Niwaeleze kitu kimoja risk za kumpa mtu mmoja nishati bure katika sekta ya simenti cost kubwa ni nishati the main cost ni nishati. Sasa huyu unampa bure hawa wengine kumi? Twiga hana wafanyakazi? Tembo hana wafanyakazi? Simba hana wafanyakazi? Sasa palipokuwa na makandokando yote nilichokuwa nawaficha ndio hicho,” alisema Mwijage.

https://youtu.be/zYFr0qW47V4

“Kama wewe ni mlezi wa wana au kama wewe ni refarii lazima uwanja uwe sawa kinyume cha hapo burudani haitakuwepo. Tutakata bei kusudi watu wafaidike lakini tutahakiisha na viwanda vingine vinaendelea kufanya kazi. Namsihi yeyote anayetaka kununua gesi akanunue gesi. Halafu ngoja nikueleze mtu anaweza kukwambia gharanma kubwa, wote wakinunua mkaa wa mawe ule na gesi ile soko si lile lile!” alifafanua.

BY: EMMY MWAIPOPO

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents