Habari

Vifo vilivyotokana na mafuriko Tanga vyafikia 14, Wananchi walala juu ya miti kujinusuru

Watu 14 mpaka sasa wameripotiwa kupoteza maisha kufuatia mvua kali zinazoendelea kunyesha mkoani Tanga, Katika wilaya ya Handeni na maeneo mengine ya mkoa huo.

Juzi mkuu wa Wilaya ya Handeni, Godwin Gondwe alisema watu 10 wamefariki baada ya gari walilokuwa wakisafiria kutumbukia kwenye mto kutokana na barabara kukatika, Huku mtu mmoja mwingine akisombwa na maji.

Jana Jumapili Polisi walithibitisha kupatikana mwili mmoja katika kitongoji cha bwawani kata ya Sindeni, na miili ya watoto wawili iliyokutwa mtaa wa Wandama kata ya Kwenjugo wilayani Handeni na idadi kamili mpaka sasa ya watu waliofariki kufikia 14.

Naye, Ofisa habari  wa Jeshi la Uokoaji na Zimamoto wilayani Handeni, Joan Luvena, amesema juzi watu 51 walilala juu ya miti katika mtaa wa Kwamaraha kutokana na makazi yao kuzingirwa na maji.

Miili yote ya marehemu imehifadhiwa katika Hospitali ya Wilaya ya Handeni mkoani Tanga, Ikisubiri mipango ya mazishi.

Chanzo: Mwananchi

 

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents