Bongo5 Makala

Vijana wengi hawajaandaliwa kuwa na malengo kwenye taaluma zao

Tunaishi kwenye nchi ambazo unazaliwa, unakua na unaambiwa elimu ni ufunguo wa maisha wengine mpaka wanazeeka hawajaweza kuona ufunguo huo ingawa wamesoma vizuri na kufanya kazi.

black-teens

Labda ni mimi sikuelewa walivyosema elimu ni ufunguo wa maisha. Kitu ambacho kinaendelea kushangaza ni kwamba vijana wengi wanakwenda shule ila hawajui hatima yao ni nini na wanasubiri serikali ifanye mambo au itoe ajira fulani hapo ndipo wanajua wamefika. Kitu kinachonifanya nijue vijana wengi hawana malengo au hawajaandaliwa ingawa wanapewa shahada na vyeti mbalimbali ni pale tu utakapowauliza ‘una mpango wa kufanya nini baada ya kumaliza shahada au elimu hii?’ Majibu utakayo kutana nayo, wewe mwenyewe utamalizia.

Vijana wengi wanachojua usalama wa ajira zao ni serikalini, hivyo wanatafuta kazi serikali ili wasipate shida wakistaafu. Maisha yamebadilika ingawa wengine bado wanawaza kama zamani. Huwezi kuamini haya ukiwa hapa mjini Dar es Salaam. Ukibahatika kwenda nje ya Dar ndipo utagundua kazi bado ipo. Nilibahatika kusikiliza maongezi ya vijana wawili ambao wanasema watafurahi sana wakipata nafasi ya uaskari au ualimu kwao maisha yatakuwa shwari kabisa. Si vibaya kuwa askari au mwalimu lakini najaribu kukupa picha ya vijana wetu wengi. Tunaona nini au hatuwezi kuona zaidi ya sehemu fulani hivyo tunabakiwa na mawazo mgando ambayo hayawezi kututoa hapa tulipo.

Hivi karibuni nilipata kisa cha kijana mmoja aliyepata kazi nzuri kwenye shirika moja hapa jijini (jina namhifadhi) ilimbidi kuacha kazi ya kitu alichosomea kwa kushindwa kufanya kazi kwa ufanisi. Ukweli ni kwamba cheti chake ni kizuri sana ila hawezi kufanya kazi kwa kuwa ni mgumu wa kuelewa. Miezi mitatu ya kufanyiwa tathmini ya kazi akatoka bila kitu. Ukieliza alifaulu vipi? Je mafunzo kwa vitendo alipitaje? unashindwa kupata majibu, tatizo nini?

Tunahitaji mfumo utakaosaidia wimbi kubwa la vijana ambao wako mashuleni na vyuoni waweze kustahimili mabadiliko makubwa na kuangalia upya malengo yao kitaaluma ili waweze kupambana na maisha vizuri. Kukosekana na mfumo wenye kusaidia vijana kusoma kwa malengo kunasababisha kuwa na vijana wengi wasomi wasiokuwa na ujuzi mahsusi kwenye nyanja fulani fulani hivyo kujikuta wanapata shida kwenye soko la ajira kutokana na ushindani kuwa mkubwa na unaohitaji ujuzi katika utendaji wake.

Awali Mwaisanila

A Personal Career Development specialist, passionate about empowering emerging generations of student, graduates and working class.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents