Bongo5 MakalaFahamuHabari

Aliyebadili maisha ya Ronaldo, anaishi maisha ya kifahari

Katika binadamu ambaye Ronaldo hawezi kumsahau kwenye maisha yake ni huyu mwamba wa kuitwa Albert Fantrau, ndio mtu aliyemfanya Ronaldo aheshimike sasa hivi, henda bila yeye Cristiano Ronaldo angekuwa muuliza bagger kwenye migahawa ya huko Madeira nchini Ureno.

CR7 anasema: – “Lazima nimshukuru rafiki yangu Albert Fantrau kwa mafanikio yangu. Tulicheza pamoja kwenye klabu ya vijana eneo tulipozaliwa huko Madeira.

Kuna siku Watu kutoka Sporting walifika kwenye timu yetu ya vijana, waliona wachezaji wengi lakini walikuwa wanatafuta mfungaji, na katika wafungaji hao al;ikuwepo mimi na rafiki yagu Albert Fantrau, walituambia kwamba yeyote atakayefunga mabao zaidi atakubaliwa kwenye Academy yao”.

“Tulishinda mchezo ule 3-0, nilifunga bao la kwanza, kisha Albert akafunga kwa kichwa, na la tatu lilikuwa bao ambalo lilimvutia kila mtu. Albert alipata mpira na kubaki yeye na  mlinda mlango.

Nilikuwa nikikimbia karibu yake na alibaki yeye na mpira kuutia wavuni, alichohitaji kufanya ni kuuweka mpira kwenye wavu iliyokuwa tupu ili afunge goli la pili haliyakuwa mimi nina goli moja.

Angefunga ina maana yeye ndio angechukuliwa nna Sporting Lakini cha kushangaza alinipa pasi na mimi nikafunga.
Nilikubaliwa kwenye Academi ya Sportinng Baada ya mechi, nilimwendea na kumuuliza “kwanini umefanya vile akajibu; “Wewe ni bora kuliko mimi inngawa hata mimi nilioa yeye ni bora kuliko mimi”

Miaka kadhaa baadaye, mwandishi wa habari alikwenda nyumbani kwa Albert, na kuuliza kama hadithi hiyo ilikuwa ya kweli. Alithibitisha.
Pia alisema kuwa taaluma yake kama mchezaji wa mpira iliisha baada ya mechi hiyo na sasa hana kazi. “Lakini nyumba nzuri kama hii, gari nk umeipata wapi?

Ulionekana kuwa mtu tajiri. Pia unatunza familia yako… yote yanatoka wapi? Albert alijibu kwa kiburi; kutoka kwa Cristiano.

Sasa hivi Albert Fatrau ni tajiri na anaishi maisha ya kifahari na ni mtu wa karibu wa Ronaldo na familia yake, inaelezwa kila anachohitaji Cristiano Ronaldo humpatia, hii ni shukrani tu kwa sababu mafanikio ya Ronaldo yote yametokana na upendo wake.

CHA KUJIFUNZA: usimsahau mtu aliyekuamini na akakupa mkono wa kusaidia maishani.

Imeanndikwa na @el_mando_tz

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents