Promotion

Wafanyabiashara kuungwanishwa na huduma mpya ya Intaneti

Wafanyabiashara kuunganishwa na huduma mpya ya intaneti ya gharama nafuu ya kampuni ya mawasiliano ya Vodacom Tanzania ili kuwarahisishia mawasiliano katika biashara zao ambapo gharama ya kuunganishwa zinawezesha unafuu wa shilingi 330,000/-

Huduma hii iliyolenga kuwarahishia mawasiliano wafanyabiashara pia inawawezesha kufurahia huduma ya internet yenye kasi kubwa kutoka mtandao wa Vodacom.

Huduma hii ya aina yake nchini inawezesha mteja kujipatia Kbs256 kwa gharama ya shilingi 100,000/-kwa mwezi ikiwemo na kodi ya ongezeko la thamani ambapo pia wanaweza kujipatia Mbps 2 kwa mwezi kwa gharama ya shilingi 200,000/- na huduma hizi zote mbili zinawawezesha kutumia internet bila kikomo.

Wateja wataunganishwa na huduma hii kutokana na mahitaji yao na watafungiwa vifaa vya kisasa vya uwezeshaji wa internet kwa kadri ya watumiaji watakaotumia huduma hii kwenye biashara au taasisi.
“Kwa watakaohitaji huduma hii wakaingia mkataba maalumu na kampuni ya Vodacom ambao utadumu kwa kipindi cha miaka 2”.Alisema Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na Uhusiano wa Vodacom Tanzania, Jacquiline Materu.

Alisema kuwa kampuni yao imekuja na huduma hii maalumu kwa kuwa wakati wote inaleta ubunifu wa huduma zinazoendana na mahitaji ya wateja wake lengo kubwa likiwa ni kuwapatia huduma za uhakika za mawasiliano na za gharama nafuu ili kuwarahisishia maisha na kuwawezesha kufurahia intaneti yenye kasi kubwa nchini kutoka Vodacom.

Kupata huduma hii anachotakiwa kufanya mteja ni kutuma maombi kwenye barua pepe ya [email protected].

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents