Habari

Wafanyakazi 16 wa Quality Group kusomewa mashtaka Machi 24

Wafanyakazi 16 wa kampuni ya Quality Group Ltd, inayomilikiwa na mfanyabiashara maarufu Yusuph Manji, watasomewa maelezo ya awali katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Machi 24 mwaka huu.

Mwendesha Mashtaka wa Uhamiaji, Method Kagoma leo amemueleza Hakimu Mfawidhi, Cyprian Mkeha kuwa upelelezi wa kesi hiyo umekamilika na akaomba tarehe ya kuwasomea maelezo ya awali washtakiwa hao.

Idadi hiyo imefikia 16, baada ya Kagoma kuwaunganisha Meneja mradi Jose Kiran, katibu wake Prakash Bhatt wanaokabiliwa na tuhuma za kukiuka amri ya Ofisa uhamiaji, na kujaribu kutoroka na washtakiwa wengine 14.

Jose na Prakash wanadaiwa kuwa Februari 20, 2017, wakiwa raia wa India na waajiriwa wa Quality Group Ltd, walimzuia ofisa wa Uhamiaji kufanya kazi zake na kwamba walikataa kuripoti katika ofisi za Uhamiaji zilizopo jijini Dar Es Salaam kwa kujaribu kutoroka nchini Tanzania kwa kupitia mpaka wa Horohoro.

By: Emmy Mwaipopo

Chanzo: Mwananchi

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents