Habari

Makonda kuwa mgeni rasmi kwenye maadhimisho ya siku ya wanawake duniani

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika maadhimisho ya siku ya Wanawake Duniani yanayotarajiwa kufanyika leo hii, katika uwanja wa Mwembeyanga Temeke Jijini Dar es Salaam.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Jumanne hii maadhimisho hayo yataongozwa na maandamano ya Wanawake na wadau mbalimbali, na yataanzia katika Shule ya Msingi Mabatini kuelekea viwanja vya Mwembeyanga.

Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani Mwaka huu yanaongozwa na kauli mbiu isemayo “Tanzania ya viwanda, Wanawake ndio Msingi wa Mabadiliko ya Kiuchumi”.

Kauli mbiu hiyo inalenga kuikumbusha jamii kuhusu umuhimu wa kujenga mazingira wezeshi kwa Wanawake hasa kutambua mchango wao katika kuleta Maendeleo yao na ya jamii kwa ujumla.

Taarifa hiyo pia imeikumbusha jamii kuhusu wajibu wake ikiwa ni pamoja na kuwashirikisha, kuwaamini na kuwapa Wanawake haki sawa katika nafasi za Elimu, Uchumi na uongozi ili wawe chachu ya mabadiliko yenye lengo la kuifanya Tanzania kuwa nchi ya viwanda.

Maadhimisho hayo yataambatana na maonesho ya kazi za ujasiriamali yanayoendelea katika uwanja wa Mwembeyanga, ambapo Asasi za kiraia na vikundi mbalimbali vya wanawake vitaonesha bidhaa zao.

By: Emmy Mwaipopo

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents