Habari

Wafungwa wawili warekodi na kutoa Album wakiwa Magereza Kenya

Wafungwa wawili katika gereza la Migori GK lililopo wilayani Migori nchini Kenya wameachia albam ya Hip-hop wakiwa gerezani.

Wafungwa hao Calvin Ochieng’ Bunde aka Lil’ Veen na mwenzie Eric Nyakundi aka Erico wametoa albam hiyo yenye jumla ya nyimbo sita.

“Albam hii inayoitwa ‘Reformed’ imetayarishwa na Fountain Studios na kugharamikiwa na gereza hilo baada ya kugundua vipaji vyao na hitaji lao la kutaka mabadiliko gerezani” alisema Peter Ayuka msimamizi wa dini gerezani.


“Kama sehemu ya kubadilika kwao, albam hiyo itakuwa kitu muhimu cha kuwafanya wawe wananchi safi na pia kuwapatia kipato,” alisema.

Albam hiyo yenye mchanganyiko wa Hip-hop na slow Genge rap, imezungumzia mabadiliko gerezani, maisha ya jela na maisha katika jamii.

Miongoni mwa mabadiliko wanayotaka ni pamoja na ongezeko la saa za kusalimiwa na ndugu na muda zaidi wa kufanya mazoezi.

Wafungwa hao wanatumikia kifungo cha miaka mitatu jela baada ya kupatikana na hatia ya kumiliki na kusafirisha fedha bandia katika matukio tofauti.

Erico alikamatwa akisafirisha fedha hizo kutoka Sirari (Tarime) kwenda Busia wakati Lil’ Veen alikuwa akizisafirisha fedha hizo kutoka Rangwe hadi Migori ili kushoot video.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents