Burudani

FID Q: Nikistaafu Muziki, Ningependa kuwa kama Profes Shivji


Rapper mashuhuri nchini Tanzania, Fareed Kubanda aka Fid Q amesema kama akistaafu kufanya muziki angependa kuwa Profesa kama alivyo Profesa Issa Shivji.

Profesa Shivji ni mhadhiri Mstaafu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam katika masuala ya sheria.

Fid ambaye anajulikana sana kwa utunzi wa mashairi mazito, alikuwa akijibu swali la shabiki katika utaratibu aliojiwekea kila weekend wa kujibu maswali kupitia Twitter.

Kuhusu swali lililomuuliza kama ana mpango wowote wa kujiingiza kwenye siasa kama walivyofanya wasanii wengine husasan Joseph Mbilinyi aka Sugu ambaye ni mbunge wa Mbeya mjini, Fid aka Ngosha amesema bado hana mpango huo kwa kujibu, “bado lakini juzi nilikutana na msafara wa John Mnyika nikavutiwa na zile shamrashamra!”

Rapper huyo kutoka Mwanza anayejulikana kwa kuwa msomaji mzuri wa vitabu husasan vya filosofia amemtaja Mwalimu Julius Kambarage Nyerere kama mwanafilosofia anayempenda zaidi katika muda wote (all time favourite philosopher).

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents