Habari

Wahamiaji 150 watelekezwa kwenye lori Mexico

Zaidi ya wahamiaji 150 kutoka Amerika ya Kati wamekutwa wametelekezwa kwenye lori lililokuwa limefurika wahamiaji hao kusini mwa Mexico, mamlaka zimesema.

Wahamiaji hao 144 waliokuwa wanatokea Nicaragua, sita wakiwa ni raia wa Nicaragua na watatu wa Salvador walikutwa kwenye lori hilo lililotelekezwa karibu na barabara kuu katika ukaguzi wa kawaida hii ikiwa ni kulingana na msemaji wa mkoa wa Chiapas.

Baada ya kugundulika wahamiaji hao walipatiwa matibabu na chakula kabla ya kukabidhiwa kwa mamlaka za uhamiaji, amesema msemaji huyo.

Maafisa wa Chiapas mji unaopakana na Guatemala wameimarisha juhudi za kuwasaka wahamiaji wanaosafiri kwenye malori moja ya njia hatari zaidi inayotumiwa na wafanyabashara haramu ya binaadamu nchini Mexico.

Related Articles

Back to top button