Habari

Wadaiwa sugu NHC watii agizo la Rais Magufuli

Shirika la Nyumba la Taifa NHC, limekusanya zaidi ya shilingi bilioni 5 na milioni 981 kutoka kwa wadaiwa sugu ambao ni asasi za serikali baada ya Rais John Magufuli kuagiza wadaiwa hao kulipa ndani ya siku 7.

raymond-mndolwa
Mkurugenzi wa Utawala na Usimamizi wa NHC, Raymond Mndolwa.

Mkurugenzi wa Utawala na Usimamizi wa NHC, Raymond Mndolwa amesema fedha hizo ni kati ya bilioni 9.346 zilizokuwa zinadaiwa kutoka wizara na taasisi za serikali huku akidai fedha hizo zitaelekezwa katika ujenzi wa nyumba 300 mjini Dodoma.

“Kwa mara ya kwanza shirika la nyumba limeshuhudia kulipwa kwa idara na taasisi za serikali na baada kutokana na maagizo yake yale na maelekezo yake yale tumeweza kukusanya shilingi bilioni 5 milioni 981 fedha hizi zimepatikana kipindi kile ambacho muheshimiwa rais alitoa maelekezo yake,” alisema Mndolwa.

“Tunampongeza sana na tunamshukuru sana lakini pamoja na hayo ili kuonyesha umuhimu wa kazi ya mheshimiwa rais anayoifanya ni suala zima la kuihamishia serikali Dodoma shirika la nyumba la taifa kupitia mkurugenzi wake mkuu imeamua fedha hizi zote ambazo zimekusanywa kama sehemu ya madeni kuzielekeza Dodoma kama sehemu za makazi na ujenzi wa nyumba ambazo zitakuwa nyumba mia 3,” aliongeza.

BY: EMMY MWAIPOPO

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents