Michezo

Huu ndio muda atakaokaa nje ya uwanja Diafra Sakho

Taarifa zimetoka kuwa mchezaji wa klabu ya West Ham United Diafra Sakho, atakua nje ya uwanja kwa muda wa wiki sita kutokana na maumivu ya paja.

3acdef5800000578-0-image-m-13_1480425595344

Sakho ambaye ana miaka 26, alitolewa uwanja dakika ya 66, katika mchezo wa ligi kuu ya Uingereza dhidi ya Man United wikiendi iliyopita.

Mshambuliaji huyo alirejea uwanjani katika mchezo huo baada ya kuwa majeruhi kwa muda na kuifungia timu yake bao la kuongoza.

Kocha wa West Ham Slaven Bilic amesema, “Ni pigo kubwa kwetu.” Kuumia kwa nyota huyu wa timu ya taifa ya Senegal kunatia mashaka kama ataweza kushiriki michuano ya kombe la mataifa ya Afrika yatayofanyika mwezi January, mwakani.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents