Habari

Waislam watakiwa kujikomboa kiuchumi, mbinu zahainishwa (Video)

Waislam nchini wametakiwa kuanzisha jukwaa la biashara ‘Muslims Commerce Chamber’ mwamvuli ambao utaongonisha waislamu kibiashara nchi nzima na kutoa mafunzo pamoja na kuwaongamisha masoko mapya ya biashara.

Hayo yamebainishwa na Katibu Mkuu wa Taasisi ya Dhinurain Islamic, Sheikh Shamsi Elmi wakati akitoa mada katika Mkutano wa Wana Taaluuma wa Kiislamu Tanzania (TAMPRO) ambao wamedai Waislamu wana hali mbaya kiuchimu na lengo la Mkutano huo ni kukomboa uchumi wa Waislamu Tanzania.

Dr. Elmi amesema kuna wafanyabiashara wengi wanashindwa kupiga hatua kutokana na kukosa mafunzo na njia ambazo zitawawezesha kuwafikisha mbali katika biashara zao.

“Kama tunataka kuangalia uchumi wetu tuangilie uchumi wa wafanyabiashara wadogo wadogo, huku chini kuna watu wanakosa hata mlo mmoja wa siku, tukiwawezesha hawa au tukiwafikia tutakuwa tumeukomboa Umma wa Waislam,” alisema Elmi

Awali mwanazuoni huyo alibainisha jambo lingine ambayo linatakiwa kuangaliwa ili kufungua biashara kwa waislam ni kuwa na bodi ya halali ambayo itakuwa inatoa vibali vya biashara ambazo zimekidhi matakwa ya dini ya kiislamu.

Akitolea mfano amesema kunatakiwa kuwe na saloon za kiislam, mabucha pamoja huduma zingine ambazo zimethibitishwa na hiyo bodi kwani kuna waislamu wengi wanaogopa
kwenda kwenye huduma hizo kutokana na mazingira ambayo sio rafiki kwa dini ya Kiislam.

Naye Dr. Ali Said Sunkar ambaye ni Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Kiislam Kenya amewataka vijana wawe na shauku ya kutaka kufanikiwa kutokana na fursa mbalimbali.

“Hali ya uislam ni mbaya na kwa kufanya hivi kuna namna nambo yanaweza kuboreka. Zimetajwa baadhi ya njia lakini vijana ndio walengwa ambao wanatakiwa kuelimishwa na kupewa fursa mbalimbali,” aliongeza.

Waandaji wa mkutano huo walisema kupitia Haji Mrisho Rubibi ambaye ni Katibu wa TAMPRO amesema wanaendelea kufanya mikutano hiyo ili kuhakikisha jamii ya kiislam inakomboka kutoka na fursa mbalimbali.

“Kuna fursa nyingi katika sekta ya kilimo, uvuvi pamoja na biashara ndogondogo hivyo mkutano huu utakuwa na maadhimio ya nini kifanyike ili tunavyokutana tena tuone hatua ambazo tumezipiga,” alisema Rubibi.

Written and edited by @yasiningitu

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents