Habari

Waislamu waanza ibada ya Hajj, Makkah

Ibada ya hajj kwa waumini wa dini ya kiislamu inaanza rasmi hii leo katika mji mtakatifu wa Makkah nchini Saudi Arabia.
Maelfu ya waumini wamekusanyika katika mji huo wakitokea nchi mbali mbali duniani

Ibada ya Hajj ni nguzo ya mwisho katika nguzo tano za imani ya kiislamu na ni ibada inayohimizwa kufanywa na kila muumini aliyekuwa katika uwezo wa kiafya na kiuchumi.

Hii leo katika mji mtakatifu wa Makkah maelfu ya waumini wamekusanyika kuanza rasmi ibada hiyo ambayo tangu lilipozuka janga la virusi vya Corona takriban miaka mitatu iliyopita ndiyo inayofanywa na watu wengi baada ya Saudi Arabia mwezi Aprili dkutangaza  kuruhusu jumla ya waumini milioni moja kushiriki.

Mwaka 2020 na 2021 Saudi Arabia ilizuia raia kutoka nchi za kigeni kushiriki ibada hiyo kutokana na mripuko wa janga la Corona lililopiga duniani.

Hii ni ibada ambayo kwa baadhi ya waumini kwao ni ya kihistoria na mmoja wa waumini hao ni Adam Mohammed raia kutoka nchini Uingereza mwenye umri wa miaka 53,mhandisi wa masuala ya umeme ambaye amegonga vichwa vya habari kwa kipindi cha miezi kadhaa baada ya kuianza safari yake ya kuelekea Makkah kwa miguu mwaka jana.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents