Habari

Waisrael waandamana usiku, wamtaka Waziri Mkuu ang’atuke

Maelfu ya Waisrael wameandamana jana usiku kote Israeli dhidi ya Waziri Mkuu Benjamin Netanyahu, wakiendelea na kampeni yao dhidi yakiongozi huyo licha ya serikali kupiga marufuku mikusanyiko ya watu katika juhudi mpya za kuzuia kuenea maambukizi ya virusi vya corona.

Wakati Netanyahu amesema marufuku hiyo ni kwa lengo la kulinda usalama wa raia, waandamanaji wanamshutumu kwa kutaka kukomesha harakati zao.

Waandamanaji hao wamekuwa wakikusanyika nje ya nyumba ya Netanyahu mjini Jerusalem kila wiki kwa zaidi ya miezi mitatu, wakimtaka ajiuzulu.

Waandamanaji wanasema Netanyahu hapaswi kuwa Waziri Mkuu wakati anashtakiwa kwa madai ya ufisadi.

Aidha wanamlaumu pia kwa kushindwa kuushughulikia ipasavyo mgogoro wa virusi vya corona, ambao umeharibu uchumi wa nchi hiyo. Wengi wa waandamanaji ni Waisrael vijana ambao wamepoteza kazi kutokana na janga hilo.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents