Habari

Walioshambulia kanisani walijificha katikati ya waumini – Polisi Nigeria

Polisi nchini Nigeria wanasema watu wenye silaha walioua zaidi ya watu 20 katika kanisa siku ya Jumapili walijifanya kuwa washirika wa kanisa hilo.

Msemaji wa polisi amesema kuwa washambuliaji walilipua vilipuzi ndani ya jengo la kanisa, huku wengine wakifyatua risasi nje ya jengo la kanisa hilo.

Bado haijabainika ni kwanini walifanya mashambulizi hayo katika mji wa kusini -magharibi wa Owo.

Polisi pia bado hawajatangaza idadi rasmi ya waliofariki.

Umoja wa Mataifa nchini Nigeria umesema “unalaani vikali shambulio hilo dhidi ya waumini”, kulingana na taarifa ya msemaji wa katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifakwa niaba ya Mratibu wa shughuli za Umoja huo nchini Nigeria, Mattias Schmale.

Bw Schmale ametoa wito wa utulivu na kuomba wahusika wa shambulio hilo kuchukuliwa hatua za sheria.

Shambulio hilo lilitawala mkutano wa chama tawala cha Nigeria, ambacho kimeanza mchakato wa kumchagua mgombea ajaye wa urais katika uchaguzi mkuu ujao.

Rais Muhammadu Buhari hawezi kugombea tena, baada ya kuhudumu kwa mihula miwili.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents