BurudaniHabari

Wamarekani waanza kuuhofia muziki wa Afrobeats, waamini unaenda kuiua Hip Hop ya Marekani

Mchekeshaji kutoka nchin i Marekani Lil Duval amezua gumzo mitandaoni na kushambuliwa sana baada ya ku-tweet na kusema kuwa

“Afrobeats inaweza kuwa kifo cha hip hop kama tunavyojua,” baada ya kuona watu wamemshambulia sana hakubadili kauli yake bali aliongeza Tweet nyingine akisema

“Sikuwa nikisema hip hop imekwisha nilisema ‘hip hop kama tunavyoijua’ nikimaanisha kama ilibadilika kuwa kitu kikubwa zaidi,” alifafanua.

Kauli kama hizi sio kwamba Duval amekosea kuongea bali wengi wameshangazwa na kitendo cha wasanii kutoka Afrika kupata nafasi ya klutumbuiza kwenye tukio kubwa la NBA ALL STAR ambapo wasanii kutoka Afrika kama Burna Boy, araema na Tems walitoa burudani.

Mbali na hilo tukio wasanii wengi wa Marekani wamekua wakifanya remix za yimbo za wasanii kutoka Nigeria mfano Come down ya Rema ambapo alim shirikisha Selena Gomez lakini pia Monalisa ya Lojay x Sarz wakimshirikisha Chris Brown lakini pia nyimbo za wasanii kutoka Nigeria kufannya vizurio Marekani kama Essence ya Wizkid, Tmes Free mind na nyingine.

Vitu kama hivi vimepelekea mijadala mikubwa Marekani wakihisi muziki wao pendwa wa Hip Hop wanauona kama unaelekea kufa na nafasi hiyo inachukuliwa na AFROBEATS.

Unahisi maoni ya Lil Duval yapo sahihi??

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents