Habari

Wanaume waonywa saratani ya matiti, Watakiwa kujichunguza kwani nao wapo hatarini kuugua

Kwa mitazamo ya watu wengi hapa nchini, Huamini kuwa ugonjwa wa saratani ya matiti unawapata wanawake pekee lakini ukweli ni kwamba hata wanaume pia wanaweza kupatwa na ugonjwa huo japo ni nadra sana.

Kufuatia ukweli huo, Wanaume wote nchini wameshauriwa kuwa na utamaduni wa kujichunguza matiti ili kubaini viashiria vya saratani ili wasichelewe kuanza matibabu endapo wakibainika na ugonjwa huo.

Wito huo umetolewa na daktari bingwa wa Saratani, Sikudhani Muya wakati wa uchunguzi wa saratani ya matiti na utoaji elimu juu ya ugonjwa huo uliofanyika jana katika hospitali ya Mloganzila.

Saratani ya matiti kwa wanaume ni aghalabu, inaweza kutokea ukapata mgonjwa mmoja kwa miaka 10, lakini wanawake ni tatizo linalowasumbua zaidi,” amesema Dkt. Muya.

Dkt. Muya ameeleza kuwa licha ya wanawake kuwa waathirika wakubwa wa saratani ya matiti, Wapo pia wanaume wanaopata ugonjwa huo, lakini huchelewa kujigundua kutokana na maumbile yao.

Kwa upande wa Serikali, Naye Naibu Waziri wa Afya, Dkt. Faustine Ndungulile amesema Serikali imeelekeza nguvu katika kupambana na saratani ya matiti kwa wanawake ambao ndio waathirika wakubwa halikadharika wanaume wanaojihisi viashiria vya ugonjwa huo kufika kwenye vituo vya afya.

Hayo yamejiri ikiwa ni muendelezo wa matukio ya kuadhimisha mwezi wa utoaji elimu ya ugonjwa wa Saratani.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents