Wasanii wa filamu kusherehekea miaka 3 ya ‘Bongo Movies’
Wasanii wa filamu nchini wanatarajia kuungana kwa pamoja mwisho wa wiki hii na kusherehekea mafanikio ya miaka 3 ya kulikamata soko la filamu nchini pamoja na kuwaenzi wasanii wa filamu waliotangulia mbele ya haki.
Baadhi ya wasanii wa Bongo Movie wakiwa kwenye picha ya pamoja
Akizungumza na E-Newz ya EATV, Mwenyekiti wa Bongo Movies, Steve Nyerere alisema ingawa tukio hilo litahudhuriwa na wasanii mbalimbali pia kutakuwa na burudani kutoka kwa bendi ya FM Academia.
“Siku ya Ijumaa tutakuwa na birthday ya bongo movie kufikisha miaka mitatu (3) toka imeanzishwa na vilevile kutakuwa na burudani nyingi,kutakuwa na FM Academia,kutakuwa kuna Banana Zorro,kutakuwa kuna Linex,kutakuwa kuna Shilole,lakini vilevile katika bongo movies sisi tumekubaliana kuna watu waliofanya kazi vizuri ndani ya mwaka kwa kuwapa tuzo.”