BurudaniVideos

Wasanii wasiwe king’ang’azi kufanya hip hop ya kizamani – Mchizi Mox (Video)

Rapper mkongwe nchini, Taikuni Ally aka Mchizi Mox amesema mabadiliko kwenye hip hop ni muhimu kwasababu sio dini ambayo haiwezi kubadilika.

Akiongea na Bongo5, Mox amedai kuwa hata Marekani ambako muziki huo ndio ulianzia wamebadilika kwa kiasi kikubwa hivyo ni ajabu kuona rapper wa Tanzania akiendelea kukomaa na muziki ambao umepitwa na wakati.

Amedai kuwa wasikilizaji wa redio na watazamaji wa TV ni teenagers ambao kama rappers watawapa muziki usioendana na wakati wao, ni sawa na kutwanga maji kwenye kinu.

“Generation yetu sisi wachache sana wanasikiliza redio, wachache sana wanaangalia TV,” anasema. “Generation inayoangalia TV sasa hivi ni nyingine kabisa, teenagers kwenda twenty hivi – hao ndio wana muda na TV, wana muda na redio, kwahiyo tunawahitaji wale kuweza kutusikia sisi tunafanya nini, wao waingie kwenye soko letu, wao na wao watupe hela zao, wahudhurie kwenye matamasha yetu, wao ndio watu wanaoweza kuhudhuria matamasha kwa wingi sasa hivi,” amesisitiza.

“Ukizungumzia generation yetu sasa hivi mshkaji wangu mwingine anafanya kazi benki, mwingine anafanya kazi sijui bandari, mwingine sijui yuko zake Ulaya, kila mtu yuko busy, hana muda wa redio, hana muda wa kwenda hata kwenye matamasha yangu wakati mwingine. Kwa maana hiyo sasa mimi ninatakiwa ili niendelee kuwepo kwenye muziki basi nicheze na hawa watu wengine ambao wanachipukia niweze kuwalisha vitu vyangu niwaambukize twende sawa.”

Mchizi Mox amedai kuwa mwezi huu amejipanga kuachia wimbo na video mpya.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents