Michezo

Washindi wa tuzo za La Liga msimu wa 2015/2016

Tuzo za La Liga Award 2015/2016 zilitolewa rasmi usiku wa October 24 2016, tuzo za wachezaji na makocha waliofanya vizuri katika msimu wa 2015/2016 ndio zilitolewa huku Luis Suarez wa FC Barcelona akiwa mchezaji wa kwanza kutwaa tuzo ya mchezaji bora wa dunia, tuzo ambayo imetolewa kwa mara ya kwanza.

cvvvv

List ya washindi wa tuzo za La Liga msimu wa 2015/2016

Kocha wa Atletico Madrid Diego Simeone ametangazwa kuwa mshindi wa tuzo ya kocha bora wa La Liga.

Luka Modric wa Real Madrid amepata tuzo ya kiungo bora wa La Liga.

Marco Asensio wa Real Madrid ambaye aliyekuwa kwa mkopo Espanyol ameshinda tuzo ya mchezaji bora anayechipukia.

Golikipa wa Atletico Madrid Jan Oblak ameshinda tuzo ya golikipa bora La Liga.

Diego Godin wa Atletico Madrid ameshinda tuzo ya beki bora.

Antoine Griezmann wa Atletico Madrid ameshinda Mchezaji Bora wa La Liga aliyechaguliwa na mashabiki.

Luis Suarez wa FC Barcelona ameshinda tuzo ya mchezaji bora wa dunia wa LaLiga.

Lionel Messi wa FC Barcelona ameshinda tuzo ya mshambuliaji bora wa LaLiga.

Antoine Griezmann ameshinda tuzo ya mchezaji bora wa LaLiga.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents