Habari

Watoto wafariki kwa kula vitafunwa vilivyopikwa kwa dawa ya kuulia wadudu

Watoto wawili nchini Uganda wamefariki dunia huku wengine 11 wakipelekwa hospitali baada ya kula kitafunwa mfano wa hamri maarufu kama, Kabalagala kilichotengenezwa kwa sumu ya kuuwa wadudu badala ya mafuta, gazeti la Daily Monitor newspaper linaripoti.

Image result for uganda food Kabalagala

Vitafunwa aina ya Kabalagala

Watoto wote 13 wanatoka familia moja Budumba, magharibi mwa Uganda na kusemekana kwamba walikuwa na umri wa 5 na 6.

Gazeti hilo limeripoti kwamba watoto hao walijipikia wenyewe vitafunwa hivyo mfano wa mahamri ambavyo vinafahamika kama Kabalagala.

Watoto hao inasemekana kwamba miongoni mwa viambato walivyotumia wakati wanapika ilikuwa dawa ya kuua wadudu inayonyunyizwa kwenye matikiti maji na mbogamboga zinazokuzwa wakidhani kwamba ni mafuta.

Kulingana na gazeti hilo, watoto hao walianza kutapika na kupelekwa hospitali ya Busolwe ambapo wawili wao waliaga dunia huku wengine 11 wakiendelea kupata matibabu.

Akithiitisha kisa hicho, mkuu wa polisi wa eneo Ceasar Tusingwire alithibitisha tukio hilo.

“Watoto 13 kutoka familia moja wanashukiwa kwamba wamekula mahamri yenye sumu. Walichanganya dawa ya kuua wadudu na mafuta ya kupikia kwa bahati mbaya, “Mr Tusingwire amesema.

“Walionusurika wanaendelea vizuri lakini bado hawajapa nguvu. tunajitahidi kuhakiksha watoto wamerejea katika hali yao ya kawaida, mhudumu mmoja wa afya amesema hivyo.

Polisi imesema miili ya waliokufa inafanyiwa uchunguzi huku na kuongeza kwamba imenzisha uchunguzi kuhusiana na kisa hicho.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents