Siasa

Watu 38 wafariki katika maandamano Mynmar

Watu 38 wameuawa nchini Myanmar siku ya Jumatano katika kile ambacho Umoja wa Mataifa umeelezea kuwa “siku ya umwagikaji mkubwa wa damu” tangu mapinduzi yalipofanyika mwezi mmoja uliopita.

Mjumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Myanmar Christine Schraner Burgener, amesema kuna kanda za video za kugutusha kutoka nchini humo. Mashuhuda wanasema vikosi vya usalama vinatumia risasi halisi na zile za mpira dhidi ya waandamanaji.

Maandamano ya halaiki na visa vya vurugu vimeshuhudiwa katika maeneo tofauti nchini Myanmar tangu jeshi lilipochukua madaraka Februari mosi.

 

Waandamanaji wamekuwa wakishinikiza kukomeshwa kwa utawala wa kijeshi na kuachiliwa huru kwa viongozi wa nchi hiyo waliochaguliwa – akiwemo Aung San Suu Kyi – ambaye aling’olewa madarakani na kuzuiliwa wakati wa mapinduzi.

Mapinduzi hayo na kutumiwa kwa nguvu kuvunja maandamano yaliyofuata yamelaaniwa kimataifa, hatua ambayo ime majeshi ya Myanmar yamepuuza.

Ikiangazia vino vya situ ya Jumatano, Uingereza imetoa wito wa kuitishwa kwa mkutano wa Baraza Kuu la Usalama la Umoja wa Mataifa, huku Marekani ikisema kuwa inatafakari kuwachukua hatua zaidi dhidi ya viongozi wa jeshi la Myanmar

Ghasia za hivi punde zinajiri siku moja baada ya majirani wa Myanmar kuomba majeshi kujizuia kufanya maafa zaidi.

‘Walikuja na kuanza kutupiga risasi’

Bi. Schraner Burgener amesema karibu watu 50 wameuawa kufikia sasa “naw engine Wendi kujeruhiwa” tangu mapinduzi yalipofanyika.

Amesema kanda mojo ya video inaomuonesha polisi akimpiga mhudumu wa afya wa kujitolea ambaye hakuwa na silaha. Nyingine inamuonesha mwandamanaji akipigwa rasasi na pengine kuuawa barabarani.

“Niliwauliza baadhi ya wataalamu wa silaha na huenda wakanithibitishia, haionekani vizuri lakini inakaa kama bunduki ya polisi kumaanisha risasi zilitumika,” alisema.

Mwanahabari kutoka ndani ya Myanmar alielezea jinsi vikosi vya usalama vilivyowamiminia risasi umati mkubwa wawatu katika miji tofauti, ukiwemo mji waYangon, bila kutoa onya.

Wavulana wawili, wail na umri wa miaka 14 na 17, ni miongoni maw wale waliouwa, Shirika la watoto la Save the Children limesema. Mwanamke wa miaka 19 anasemekana kuwa miongoni mwa waliouawa.

Protesters sit in a street holding makeshift shields as they face police in riot gear, in Mandalay on 3 March 2021
Maaskari wanaaminiwa kutumia silaha dhidi ya waandamanaji

Protesters are seen in a barricade during an anti-coup protest in Yangon, Myanmar
Waandamanaji wamejenga vizuizi katika miji kadhaa kote nchini

Karibu watu Sita waliripotiwa kuuawa kwa kupigwa risasi wakati wa maandamano katika eno la Monywa katikati ya Myanmar. Wengine karibu 30 walijeruhiwa katika ghasia hizo, mwanahabari wa eneo hilo aliambia shirk la habari la Reuters.

Wahudumu wa afya wa kujitolea wameimbia shirika la habari la AFP mjini Myingyan kwamba karibu wa 10 walijeruhiwa katika eneo hilo. “Walirusha vitoa machozi, kupiga risasi za mpira na rises halisi,” they said.

“Hawakutumwagia maki ya mwasho, [hawakutoa] onyo la kututaka tuondoke, walikuja tu na kwanza kupiga risasi” mmoja wa waandamanaji katika mji huo aliambia Reuters.

Katika mji wa Mandalay, mwanafunzi mwandamanaji aliambia BBC kwamba waandamanaji kadhaa waliuawa karibu na nyumba yake.

“Nadhani kama mwendo wa saa nne au nne na nusu asubuhi, polisi na walikuja katika eneo hilo na kisha wakaanza kuwapiga risasi raia. Hawakutoa onyo lolote kwa raia.

“Walitokea tu na kuanza kupiga risasi. Walitumia risasi za mpira na pia risasi halisi kuua raia kwa njia ya kikatili.”

Jeshi haijatoa tamko lolote kuhusiana na vifo vilivyoripotiwa.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents