Burudani

Watu ndio wanapenda, si kwamba naimba mapenzi sana – Lady Jaydee

Msanii wa Bongo Flava, Lady Jaydee amesema si kweli anaimba sana mapenzi bali ni watu ndio wanapenda.

Muimbaji huyo ambaye kwa sasa anafanya vizuri na ngoma ‘I Miss You’ ameiambia TBC 1 kuwa wasanii wanaimba mapenzi kutokana na mahitaji ya mashabiki wao.

“Watu wanachopenda ndio huwa kinasikika zaidi, kwa hiyo nafikiri ndio watu huwa wanapenda mapenzi, siyo kwamba mimi ndio huwa naimba mapenzi sana,” amesema Lady Jaydee.

Katika hatua nyingine amezungumzia ongezeko la wasanii wa kike katika muziki wa Bongo Flava na kueleza kuwa;

“Nafurahi sana kwa sababu kwa kipindi kirefu kumekuwa na uhaba wa wasanii wa kike na kila tunapoenda tunaulizwa kwanini wanamuziki wa kike si wengi lakini kwa sasa kuna unafuu mabinti wameongezeka, wamejitokeza” amesema.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents