Habari

Waziri Kigwangalla atoa neno kwa Askofu Kakobe ‘inawezekana akawa na ugonjwa wa akili’

Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt. Hamisi Kigwangalla amesema ni vyema watu wakapuuza kauli zinazotolewa na kiongozi wa Kanisa la Gospel Bible Fellowship Church (GBFC), Askofu Kakobe.

Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt. Hamisi Kigwangalla

Mhe. Kigwangalla amesema huwa anasikia kauli mbalimbali kutoka kwa watu kuwa Askofu Kakobe anasumbuliwa na ugonjwa wa akili hivyo amedai kuwa watu wampuuze na kauli zake.

Kuhangaika na mtu kama KAKOBE ni kupoteza muda bure. Kuna watu wanasema inawezekana akawa na ugonjwa wa akili ‘Bipolar Disorder: Currently Mania’ ambao katika dalili zake ni ‘delusions of grandeur’ [kujisifia]. Akipelekwa mahakamani anaweza kutetewa kwa kigezo hiki na akashinda!“ameandika Waziri Kigwangalla kwenye ukurasa wake wa Twitter.

SOMA NA HII – Askofu Kakobe kuchunguzwa na TRA, ni baada ya kudai ana fedha kuzidi serikali

Kauli hiyo ya Mhe. Kigwangalla imekuja ikiwa ni wiki moja imepita tangu Askofu kakobe aanze kutoa kauli za kuukosoa utawala wa Rais Magufuli na kujinadi kuwa yeye ana pesa nyingi kuliko serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

 

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents